• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 23, 2018

  MAPEMAAA, RATIBA LIGI KUU YAANZA KUKARABATIWA…MECHI YA SIMBA NA MBEYA CITY YASOGEZWA MBELE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BODI ya Ligi imeendelea na desturi yake ya kupanga na kupangua ratiba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, safari hii wakianza mapema tu baada ya mechi za kwanza za msimu mpya.  
  Mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba SC na Mbeya City uliopangwa kufanyika Jumamosi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam umesogezwa mbele hadi Jumatatu.

  Barua ya Bodi kwenda kwa klabu za SImba SC na Mbeya City iliyosainiwa na Mtendaji wake Mkuu, Boniphace Wambura imesema kwamba mchezo huo umeasogezwa mbele kwa sababu Uwanja wa Taifa utakuwa unafanyiwa maandalizi ya fainali ya michuano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA AFCON Qualifier) ambao utafanyika Jumapili.
  Aidha, Wambura amesema mchezo kati ya Azam FC uliokuwa uanze Saa 1:00 usiku nao umesogezwa mbele na sasa utaanza Saa 2:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAPEMAAA, RATIBA LIGI KUU YAANZA KUKARABATIWA…MECHI YA SIMBA NA MBEYA CITY YASOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top