• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 30, 2018

  LUCA MODRIC NDIYE MFALME MPYA WA SOKA ULAYA

  Luka Modric ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kiume wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) 

  WASHINDI WA TUZO ZA UEFA AWARD

  Mwanasoka Bora wa Kiume wa UEFA: Luka Modric
  Mwanasoka Bora wa Kike wa UEFA: Penille Harder
  Kipa Bora wa Msimu: Keylor Navas
  Beki Bora wa Msimu: Sergio Ramos
  Kiungo Bora wa Msimu: Luka Modric
  Mshambuliaji Bora wa Msimu: Cristiano Ronaldo
  KIUNGO wa kimataifa wa Croatia, Luka Modric ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kiume wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), baada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa taji la tatu la Ligi ya Mabingwa.
  Hiyo ni baada ya kuwapiku washambuliaji wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah na w Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye pia ni Mwanasoka Bora wa Dunia.
  Ronaldo ameshinda tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Msimu uliopita akiwa na Real Madrid baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara ya sita, wakati Sergio Ramos ameshinda tuzo ya Beki Bora na Modric amechukua pia tuzo ya Kiungo Bora.
  Kipa wa Real na Costa Rica, Keylor Navas ameshinda tuzo ya nne na ya mwisho usiku huu, baqada ya kutangazwa ndiye ya Mlinda Mlango Bora wa Msimu baada ya kuipa timu yake taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Penille Harder wa Wolfsburg ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa UEFA.
  Nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, David Beckham ameshinda tuzo ya Rais wa UEFA baada ya kazi nzuri yake nzuri anayoendelea kuifanya kwa mchezo huo japo amestaafu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUCA MODRIC NDIYE MFALME MPYA WA SOKA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top