• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 22, 2018

  MTIBWA SUGAR WAIFUATA YANGA KWA HASIRA ZA KIPIGO CHA SIMBA MECHI YA NGAO MWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila amesema kwamba wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Yanga SC kesho Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Katwila amesema kwamba baada ya kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii wakifungwa 2-1 na Simba SC Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, wanataka kuanza ligi vizuri.
  “Wachezaji wote wana afya njema na wako fiti kwa ajili ya msimu mpya, nadhani jukumu lililobaki ni la kwetu kuchagua watakaowakilisha Mtibwa siku hiyo ya Alhamisi,” amesema Katwila, mchezaji wa zamani wa Mtibwa.

  Zubery Katwila (kulia) anataka ushindi dhidi ya Yanga SC kesho Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam 

  Katwila amesema anataka kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Yanga, kwani mchezo uliopita wa Ligi Kuu waliichapa 1-0, bao pekee la Hassan Dilunga aliyehamia Simba SC Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Kwa ujumla, Ligi Kuu inatarajiwa kuanza leo; Simba SC ikiwakaribisha Tanzania Prisons kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Uhuru, Ruvu Shooting na Ndanda FC Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Alliance FC na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Coastal Union na Lipuli FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na Kagera Sugar na Mwadui FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, zote zikianza Saa 10:00.
  Ligi hiyo itaendelea Alhamisi na mbali na Yanga na Mtibwa, JKT Tanzania watamenyana na KMC kuanzia Saa 8:00 mchana Uwanja wa Meja Isamuhuyo, Stand United na African Lyon Saa 10:00 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Azam FC na Mbeya City kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAIFUATA YANGA KWA HASIRA ZA KIPIGO CHA SIMBA MECHI YA NGAO MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top