• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 29, 2018

  YANGA SC WAKAMAILISHA MECHI ZA MAKUNDI AFRIKA KWA KUCHAPWA 1-0 NA RAYON KIGALI

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  VIGOGO wa Tanzania, Yanga SC wamekamilisha mechi zao za Kundi D kwa kichapo, baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Rayon Sport Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali nchini Rwanda.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee la mshambuliaji Mrundi, Bonfilscaleb Bimenyimana dakika ya 19 baada ya kumzidi maarifa Nahodha wa Yanga, Kelvin Yondan na kumchambua kipa Benno Kakolanya kutoka upande wa kulia wa Uwanja.
  Kwa matokeo hayo, Rayon inakwenda Robo Fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tisa, nyuma ya USM Alger yenye pointi 11 baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya leo 2-1 mjini Algiers. Yanga inamaliza nafasi ya mwisho kwa pointi zake nne, nyuma ya Gor Mahia yenye pointi nane. Mchezo mwingine wa Kundi D, USM Alger imeichapa 2-1 Gor Mahia Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers.

  Mabao ya Mkongo, Prince Vinny Ibara Doniama dakika ya 36 na Amir Sayoud dakika ya 81, wakati la Gor Mahia limefungwa na Jacques Tuyisenge dakika ya 83. 
  Yanga SC sasa wanarejea nyumbani Tanzania kuelekeza nguvu zao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kwani mwakani hawatashiriki tena michuano ya Afrika.
  Na watakwenda moja kwa moja mkoani Kigoma kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United Septemba 5 Uwanja wa Lake Tanganyika, kabla ya kupewa ratiba mpya ya mechi zao zijazo za Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WAKAMAILISHA MECHI ZA MAKUNDI AFRIKA KWA KUCHAPWA 1-0 NA RAYON KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top