• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 31, 2018

  UEFA KUANZISHA MASHINDANO YA TATU YA KLABU ULAYA

  SHIRIKISHO la Soka Ulaya (UEFA) limethibitisha kuwa katika mchakato wa kuanzisha mashindano mapya ya klabu, ambayo yatakuwa ya tatu baada ya Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Ulaya.
  Baraza la Taratibu za Soka lilikutana mjini Monaco kuelekea droo ya Ligi ya Mabingwa jana kujadili mambo mbalimbali juu ya namna ya kuboresha mchezo.
  Miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika kikao kilichoendeshwa chini ya Uenyekiti wa Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin ilikuwa ni kupitia muundo wa mashindano ya klabu kuanzia msimu wa 2021-2024.

  Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin aliongoza kikao jana kupitia muundo wa mashindano ya klabu Ulaya

  Gazeti la Bild la Ujerumani limerioti kwamba mara tu baada ya hapo, iliamuliwa kuanzisha mashindano ya tatu ya ngazi ya klabu chini ya Ligi ya Mabingwa na Europa League ndani ya miaka mitatu.
  Taarifa kutoka bodi hiyo ya soka Ulaya kujibu tetesi hizo imesema: "UEFA inapitia muundo wa mashindano yake katika maeneo tofauti kwa heshima hii,".
  "UEFA inajadili mawazo tofauti na Kamati ya Mashindano ya Ngazi za Klabu kabla ya uamuzi wowote kuchukuliwa juu ya mabadiliko,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UEFA KUANZISHA MASHINDANO YA TATU YA KLABU ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top