• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 25, 2018

  COASTAL UNION YAIPIGA BIASHARA 1-0 NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU, SINGIDA YAAMKA NAMFUA

  Na Mwandishi Wetu, TANGA
  TIMU ya Coastal Union  ya Tanga imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United ya Mara Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
  Ushindi huo wa kwanza kwa timu kipenzi cha Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia unawafanya mabingwa hao wa mwaka 1988 kufikisha pointi nne baada ya mechi mbili za kwanza, kufuatia kutoa sare ya 1-1 na Lipuli FC katikati ya wiki.
  Bao pekee la Wagosi wa Kaya, au Wana Mangushi katika mchezo wa leo limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Hajji Mohammed Ugando dakika ya 20. 
  Mfungaji wa bao pekee la Coastal Union leo, Hajji Ugando dakika ya 20

  Mapema dakika ya 13, Coastal Union kipa wa Biashara United, Balora Nasridine aliinusuru timu yake kufungwa baada ya kapangua mkwaju wa penalty uliopigwa na Mtenje Albano.
  Awali ya hapo, dakika ya tatu Hamisi Kanduru alikwamisha mpora nyavuni akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Adeyoum Saleh Ahmed, lakini akaambiwa alikuwa ameotea. Biashara nao wakakataliwa bao baadaye.
  Mchezo uliofuata wa Ligi Kuu, Singida United ilizinduka na kupata ushindi wa 1-0 nyumbani Uwanja wa Namfua dhidi ya Mwadui FC, bao pekee la beki Rajab Zahir dakika ya 29.  
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi nne zaidi kuchezwa, Ruvu Shooting wakimenyana na KMC Saa 8:00 mchana Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, JKT Tanzania na Lipuli FC Uwanja wa Meja Isamuhuyo, Mbweni, Dar es Salaam na Stand United na Mbao FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, zote Saa 10:00 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAIPIGA BIASHARA 1-0 NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU, SINGIDA YAAMKA NAMFUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top