• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 21, 2018

  CHILUNDA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA TENERIFE KUCHOMOA IKIPATA SARE UGENINI MECHI YA LIGI

  Na Mwandishi Wetu, TARRAGONA
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Iddi Chilunda usiku wa Jumatatu ameichezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya, CD Tenerife ikilazimisha sare ya 1-1 ugenini na Gimnastic katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Hispania, maarufu kama Segunda.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Nou Estadi de Tarragona, Chilunda aliingia uwanjani dakika ya 86 kwenda kuchukua nafasi ya kiungo Mserbia, Filip Malbasic wakati huo Tenerife ikiwa nyuma kwa 1-0, baada ya Fali Jimenez kutangulia kuifungia Gimnastic dakika ya 10 akimaliziai pasi ya David Rocha. 

  Shaaban Iddi Chilunda ametokea benchi na kuisaidia CD Tenerife kupata sare ya 1-1 ugenini na Gimnastic 

  Lakini Chilunda akiwa uwanjani ndani ya dakika 10 za mwisho pamoja na nne za nyongeza, Tenerife ikafanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya mwisho, mfungaji akiwa beki Muargentina, Lucas Elio Aveldano akimalizia pasi ya Samuel Geoffroy Camille.  
  Chilunda amejiunga na CD Tenerife mwezi huu akitokea Azam FC ya Tanzania kwa mkopo wa miaka miwili.
  Na huko amekutana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Azam FC ambao wote wameibuliwa katika akademi ya timu ya Chamazi, Farid Mussa Malik ambaye anaingia mwaka wa pili wa Hispania. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHILUNDA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA TENERIFE KUCHOMOA IKIPATA SARE UGENINI MECHI YA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top