• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 24, 2018

  SERENGETI BOYS WAPIGWA ‘NA MADOGO WA UGANDA AMBAO WATACHEZA FAINALI NA ETHIOPIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NDOTO za Tanzania kutwaa ubingwa wa michuano ya kuwania tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA AFCON Qualifier 2019) zimeyeyuka leo baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Uganda katika mchezo wa Nusu Fainali Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, Serengeti Kobs itakutana na Rwanda katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ambayo imetolewa na Ethiopia katika mchezo uliotangulia jioni ya leo Uwanja wa Taifa.
  Uganda walitangulia kwa bao la Abdul Iddi dakika ya nne, kabla ya Tanzania kusawazisha kupitia kwa Edson Mshirakandi dakika ya 11, matokeo ambayo yalidumu hadi baada ya kipindi cha kwanza.

  Kipindi cha pili, Serengeti Boys ikazidiwa nguvu na kuwaruhusu The Kobs kupata mabao mawili zaidi kupitia kwa John Alou dakika ya 76 na Amiri Njiru aliyejifunga dakika ya 90 na ushei.
  Mapema katika mchezo uliotangulia, Ethiopia iliifunga Rwanda kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 2-2 na kutinga fainali. Mechi za Fainali na Nusu Fainali zitafanyika Jumapili Uwanja wa Taifa.    
  Pamoja na kutolewa, Serengeti Boys watashiriki fainali za AFCON U17 mwakani kwa sababu wao ndiyo wenyeji.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS WAPIGWA ‘NA MADOGO WA UGANDA AMBAO WATACHEZA FAINALI NA ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top