• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 29, 2018

  SCHWEINSTEIGER ANG'ARA BAYERN IKISHINDA 4-0

  KIUNGO Bastian Schweinsteiger jana alirejea Uwanja wa Allianz Arena kwa sherehe za kuagwa, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu Julai mwaka 2015 alipoondoka Bayern Munich kuhamia Manchester United.
  Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 34, kipindi cha kwanza aliichezea timu yake, Chigaco Fire ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) kabla ya kipindi cha pili kuhamia kwenyebsafu ya kiungo ya Bayern iliyoibuka na ushindi wa 4-0. 
  Schweinsteiger bado anakumbukwa na kuheshimiwa Bavaria kufuatia misimu 17 ya kuitumikia akianzia katika akademi ya Bayern akiwa ana umri wa miaka 13 kabla ya kuwa mchezaji mkubwa wa klabu hiyo na nchi yake.

  Bastian Schweinsteiger akirushwa juu na wachezaji wenzake wa Bayern Munich baada ya kufunga bao la nne jana

  Schweinsteiger, aliyeichezea Bayern Munich mechi 500 za mashindano yote na kushinda nayo mataji 26, bado ni mchezaji muhimu kwa klabu yake ya sasa, Chicago. 
  Mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Serge Gnabry dakika ya saba, Sandro Wagner dakika ya 38, Arjen Robben dakika ya 63 na Schweinsteiger dakika ya 83.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SCHWEINSTEIGER ANG'ARA BAYERN IKISHINDA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top