• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 30, 2018

  SOUTHGATE AMTEMA YOUNG, AMCHUKUA LUKE SHAW ENGLAND

  KOCHA Gareth Southgate amemuita kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, Luke Shaw chenye chipukizi wengi zaidi, akijumuisha wachezaji 18 kati ya 23 aliokuwa nao kwenye Kombe la Dunia.
  Pamoja na hayo, kocha huyo England ameamua kumtema mkongwe, Ashley Young - aliyekuwa anaanza kwenye kikosi cha kwanza katika fainali za Kombe la Dunia - ili kumpa nafasi mchezaji mwenzake wa Manchester United, Luke Shaw.
  Southgate ameamua kuachana na akina na Phil Foden, Ryan Sessegnon na Jadon Sancho, lakini amesistiza anataka chipukizi zaidi kama akina Shaw na Joe Gomez kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa Septemba dhidi ya Hispania na Uswsi.
  Shaw hajachezea nchi yake tangu kipigo cha 1-0 kutoka kwa Ujerumani mwaka 2017, lakini safari hii amepewa mbele ya mchezaji mwenzake wa Old Trafford, Young.
  "Luke Shaw ana umri wa miaka 23 tu, Joe Gomes miaka 21 hivyo tumechukua wachezaji wadogo tena. Tunafahamu namna ambavyo chipukizi wengine wanafanya vizuri, lakini kwa baadhi yao itakuwa mapema sana kujumuishwa,"amesema Southgate.

  Gareth Southgate amemtema mkongwe, Ashley Young (kulia) na kumchukua mchezaji mwenzake wa Manchester United,  Luke Shaw (kushoto) 

  KIKOSI CHA WACHEZAJI 23 WA ENGLAND 

  Makipa: Jack Butland (Stoke City), Alex McCarthy (Southampton), Jordan Pickford (Everton) 
  Mabeki: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Joe Gomez (Liverpool), Harry Maguire (Leicester City), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Luke Shaw (Manchester United), John Stones (Manchester City), James Tarkowski (Burnley), Kieran Trippier (Tottenham Hotspur), Kyle Walker (Manchester City),
  Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Fabian Delph (Manchester City), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Raheem Sterling (Manchester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), Jesse Lingard (Manchester United), Ruben Loftus-Cheek (Chelsea)
  Washambuliaji: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Marcus Rashford (Manchester United), Danny Welbeck (Arsenal)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SOUTHGATE AMTEMA YOUNG, AMCHUKUA LUKE SHAW ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top