• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 20, 2018

  KARIUS APELEKWA KWA MKOPO MIAKA MIWILI UTURUKI

  Loris Karius anakwenda Besiktas ya Uturuki kwa mkopo wa miaka miwili 

  TAKWIMU ZA LORIS KARIUS  LIVERPOOL 

  Mechi alizocheza: 49
  Dakika alizocheza: 4,410
  Mabao aliyofungwa: 47
  Mabao aliyofungwa kwa dakika: 93.8
  Kudaka bula kufungwa: mechi 22
  Kuokoa: 90
  Asilimia alizookoa: 65.4
  Makosa aliyoyafanya na kusababisha mabao: 5 
  KIPA Loris Karius anatarajiwa kwenda kujipanga upya katika klabu ya Besiktas ya Uturuki inayomchukua kwa mkopo wa miaka miwili.
  Mlinda mlango huyo wa Liverpool amepoteza nafasi ya kudaka Anfield baada ya kocha Jurgen Klopp kumsajili kipa namba moja wa Brazil, Alisson. 
  Karius, aliyefanya makosa mawili makubwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid, alimuudhi Klopp hadi akaamua kumsajili Alisson kwa Pauni Milioni 65 na mwezi uliopita akasema katika ziara ya Marekani alikuwa hafahamu juu ya uamuzi huo wa kocha wake.     
  Klopp ana uhusiano mzuri na Karius na alitaka mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 24, aliyemsajili kutoka Mainz kwa Pauni Milioni 5 mwaka 2016 kupata mafanikio zaidi katika Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KARIUS APELEKWA KWA MKOPO MIAKA MIWILI UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top