// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BEKI WA REAL MADRID, URENO AHUKUMIWA MIEZI SABA JELA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BEKI WA REAL MADRID, URENO AHUKUMIWA MIEZI SABA JELA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Saturday, October 07, 2017

  BEKI WA REAL MADRID, URENO AHUKUMIWA MIEZI SABA JELA

  BEKI wa zamani wa Real Madrid, Ricardo Carvalho amehukumiwa kifungo cha miezi saba jela kwa kosa la kukwepa kodi wakati anachezea klabu hiyo ya Hispania.
  Pamoja na hayo,m mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea, ambaye ameichezea mechi 89 Ureno hatakaa gerezani hata sekunde moja, kutokana na sheria za Hispania, mtu anayehukumiwa kifundo cha chini ya miaka miwili kwa mara ya kwanza hafungwi.
  Carvalho alichezea Real kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 chini ya kocha Jose Mourinho, na makosa hayo anadaiwa kuyafanya kati ya mwaka 2011 na 2012.
  Ilikuwa ahukumiwe kifungo kirefu cha mwaka mmoja na faini ya Pauni 286,824, lakini ikapunguzwa hadi miezi saba na kulipa Pauni 127, 979.
  Ricardo Carvalho amehukumiwa kifungo cha miezi saba jela kwa kosa la kukwepa kodi wakati anachezea Real Madrid nchini Hispania PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Carvalho, mwenye umri wa miaka 39 sasa, alipunguziwa adhabu kwa kukiri kosa na kuahidi kulipa kiasi kamili alichotakiwa, ambacho ni Pauni 489,242.
  Beki huyo wa kati anaendelea kucheza soka kwa kiwango kizuri ingawa umri 'umempa mkono' na alikuwemo kwenye kikosi cha Ureno kilichotwaa Kombe la Euro mwaka 2016. Kwa sasa anachezea klabu ya Shanghai SIPG ya Ligi Kuu ya China.
  Carvalho anakuwa mchezaji mwingine wa La Liga kukutwa na hatia ya ya kukwepa kodi baada ya Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Lionel Messi.
  Messi na baba yake, Jorge walikutwa na hatia Julai mwaka 2016 ya makosa matatu ya kukwepa kodi Hispania jumla ya Pauni Milioni 3.59 kwa kuficha mapato yaliyotokana mauzo ya haki za matumizi ya picha zake kati ya mwaka 2007 na 2009.
  Alihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela na kulipa faini ya Pauni 210, 000, lakini kama Carvalho hakutukumia kifungo jela.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI WA REAL MADRID, URENO AHUKUMIWA MIEZI SABA JELA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top