// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PLUIJM: MAJERUHI WALITUPUNGUZA KASI, ILA SASA TUPO KAMILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PLUIJM: MAJERUHI WALITUPUNGUZA KASI, ILA SASA TUPO KAMILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, September 12, 2017

  PLUIJM: MAJERUHI WALITUPUNGUZA KASI, ILA SASA TUPO KAMILI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba hawakuwa na mwanzo mzuri sana katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutokana na kukabiliwa na majeruhi, lakini kwa sasa mambo ni mazuri.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu mjini Dar es Salaam leo kutoka Dodoma, Pluijm amesema kwamba walikuwa wana majeruhi katika mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu, lakini sasa wamepona na wanarudi.
  Pluijm amesema mchezaji mmoja tu kwa sasa anabaki kwenye orodha ya wachezaji majeruhi, ambaye ni kipa mkongwe, Ally Mustafa ‘Barthez’, lakini wengine wote kwa sasa wapo fiti.
  Kocha Mholanzi wa Singida United, Hans van der Pluijm amesema kwamba walianza ligi kwa kusuasua kutokana na kukabiliwa na majeruhi 

  “Bahati mbaya tulikuwa tuna wachezaji kadhaa majeruhi kikosini, lakini kwa sasa safi. Wengi walikuwa wanasumbuliwa na maumivu ya enka kwa sababu ya viwanja vibaya, lakini mechi ijayo wengi watarudi, wamepona,”amesema Pluijm.
  Kocha huyo wa zamani wa Yanga SC amesema kwamba Barthez kwa upande wake anataraiwa kurudi wiki ijayo. Baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbao FC mwishoni mwa wiki Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Singida United wanarudi Shinyanga kumenyana na wenyeji, Stand United Uwanja wa Kambarage Jumamosi.  
  Ikumbukwe Singida iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, iliuanza msimu kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga Agosti 26, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM: MAJERUHI WALITUPUNGUZA KASI, ILA SASA TUPO KAMILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top