• HABARI MPYA

  Friday, September 08, 2017

  MSUVA KESHO LIGI KUU MOROCCO, SAMATTA JUMAPILI UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NYOTA wa Tanzania wanaocheza nje ya nchi wikiendi hii watakuwa wanazipigania timu zao katika Ligi za nchini mwao, baada ya kurejea kutoka kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa.
  Akitoka kuifungia mabao yote Tanzania katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana katika mchezo wa kirafiki Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam – winga Simon Msuva kesho atacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola.
  Timu mpya ya Msuva, Difaa El Jadida kesho itaikaribisha Chabab Atlas Khenifra Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida Mazghan kuanzia Saa 3:00 usiku atika Ligi ya Morocco.
  Simon Msuva kesho anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola

  Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta akitoka kuiongoza Taifa Stars kushinda 2-0 dhidi ya Botswana atasafiri na timu yake KRC Genk kwa mchezo wa ugenini dhidi ya AA Gent Jumapili Uwanja wa Ghelamco-Arena kuanzia Saa 9:30 Alasiri.
  Wachezaji wengine wanacheza nje waliokuwepo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichowazima Pundamilia Dar es Salaam ni Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini ambayo Jumanne itamenyana na Chippa United katika mchezo wa PSL, Elias Maguri wa Dhofar ya Oman ambayo kesho itamenyana na Al Suwaiq katika mechi ya Kikombe na Hamisi Abdallah wa Sony Sugar ya Kenya na Farid Mussa wa Tenerife ya Hispania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA KESHO LIGI KUU MOROCCO, SAMATTA JUMAPILI UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top