• HABARI MPYA

  Friday, September 15, 2017

  MASHABIKI WA FC COLOGNE WALIVYOIWEKA ROHO JUU LONDON JANA

  MCHEZO wa Kundi H Ligi ya Ulaya kati ya Arsenal na FC Cologne ya Ujerumani ulichelewa kuanza jana kwa saa moja kwa sababu za kiusalama kutokana na vurugu za mashabiki wa timu mgeni.
  Mashabiki hao walikuwa wanafanya fujo kulazimisha kuingia uwanjani kinyume cha taratibu.
  Kiasi cha mashabiki 20,000 wanakadiriwa kusafiri kutoka Ujerumani kuingia London kuishuhudia timu yao ikiche`a michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 25.
  Hali iliyosababisha vurugu na kama si juhudi za Polisi na walinzi wa Uwanja wa Emirates athari kubwa ingetokea jana.

  Shabiki wa FC Cologne akiwa ameshika moshi mwekundu kwenye kona ya Highbury jana kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal
   
  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Mashabiki wengi hawakuwa hata na tiketi na walikuwa wanalazimisha kupewa tiketi na walinzi nje ya Uwanja wa Arsenal, hali iliyoulazimu uongozi wa klabu kufunga mageti na kuufunga Uwanja.
  Kulikuwa kuna taarifa za matukio ya ukosefu wa adabu, uvunjifu wa amani na uvunjaji wa sheria, ikiwemo mashabiki hao kukojoa ovyo mitaani na picha moja mwenye mtandao wa kijamii ilimuonyesha mtu akitokwa na damu kichwani kama amepigwa. 
  Mashahidi walisema hata viti ndani ya Uwanja wa viliharibiwa na kuna wakati ilikwishaonekana mchezo huo hautafanyika tena.
  Bahati nzuri Polisi na walinzi wa Uwanja wakafanikiwa kutuliza hali hiyo na mechi ikachezwa huku Arsenal wakitoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 3-1. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHABIKI WA FC COLOGNE WALIVYOIWEKA ROHO JUU LONDON JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top