• HABARI MPYA

  Friday, September 15, 2017

  ARSENAL WAANZA VYEMA LIGI YA ULAYA, WASHINDA 3-1 EMIRATES

  Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili dakika ya 67 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya FC Cologne ya Ujerumani kwenye mchezo wa Kundi H michuano ya Ligi ya Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Emirates, London. Mabao mengine ya The Gunners yalifungwa na Sead Kolasinac dakika ya 49 na Hector Bellerin dakika ya 81 baada ya wageni kutangulia kwa bao la Jhon Cordoba dakika ya tisa. Mechi hiyo ilichelewa kuanza jana kwa saa moja kutokana na vurugu za mashabiki wa FC Cologne PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL WAANZA VYEMA LIGI YA ULAYA, WASHINDA 3-1 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top