• HABARI MPYA

  Thursday, September 07, 2017

  MAMA HUYU 'ANAVYOMFUA' TERRY KWA MAZOEZI MAKALI

  BEKI wa zamani wa kimataifa wa England, John Terry anafanya mazoezi ya Yoga kujiweka fiti kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu ya England akiwa na klabu yake mpya, Aston Villa
  Mchezaji huyo aliyesaidia Chelsea kutwaa taji la Ligi Kuu ya England mssimu uliopita, ameposti picha tano akifanyishwa mazoezi ya Yoga na mwalimu wa kike, Ambra Vallo.
  Baada ya kucheza Chelsea kwa maisha yake yote, JT ametua Villa kumalizia soka yake. Aliwasili kwa mara ya kwanza The Blues akiwa kijana mdogo mwaka 1995 akiwa ana umri wa miaka 15 akitokea akademi ya West Ham.
  Beki wa Aston Villa, John Terry akifanyishwa mazoezi na Ambra Vallo wiki hii PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Baada ya miaka mitatu ya kucheza akademi ya Chelsea, Terry akapandishwa kikosi cha kwanza mwaka 1998, kabla ya kupelekwa kwa mkopo wa muda mfupi Nottingham Forest. Alirudi baada ya miezi kadhaa na akacheza Stamford Bridge hadi alipoondoka mwaka jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMA HUYU 'ANAVYOMFUA' TERRY KWA MAZOEZI MAKALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top