• HABARI MPYA

  Thursday, September 07, 2017

  MCGREGOR ANAVYOPOZA MACHUNGU YA KIPONDO CHA MAYWEATHER

  BONDIA Conor McGregor yuko mapumziko kwa sasa kufuatia kipigo cha Technicakl Knockout (TKO) mbele ya Floyd Mayweather mjini Las Vegas, Marekani Agosti 26.
  Nyota huyo wa UFC ameamua kupumzisha akili yake baada ya kipigo cha KO katika raundi ya 10 kutoka kwa Mayweather wiki mbili zilizopita kwa kwenda kujianika juani na familia yake.
  McGregor ameposti kwenye akaunti yake ya Instagram picha kadhaa akifurahia maisha na mwanawe wa kiume, Conor Jnr, mpenzi wake, Dee Devlin na dada yake, Aoife.
  Wakati huo huo kwa mujibu wa kocha wa McGregor, John Kavanagh, mbabe huyo wa Ireland anaweza kurejea kwenye ulingo wa UFC mwaka 2018 kwa kupigana na Nate Diaz.

  Conor McGregor yuko mapumziko baada ya kipigo cha TKO cha Floyd Mayweather mjini Las Vegas, Marekani Agosti  

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCGREGOR ANAVYOPOZA MACHUNGU YA KIPONDO CHA MAYWEATHER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top