• HABARI MPYA

  Monday, September 04, 2017

  MAJI MAJI WAPATA UDHAMINI MILIONI 150 KWA MWAKA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Sokabet leo imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na klabu ya Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wenye thamani ya Sh. Milioni 150.
  Katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Courtyard, Dar es Salaam, Mwakilishi wa kampuni hiyo nchini, Franco Ruhinda amesema kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi inayopenda michezo hivyo wataipa kipaumbele michezo mbalimbali hapa nchini ikiwa wameanza na udhamini wa mwaka mmoja kwa Maji Maji.
  Ruhinda amesema kwamba licha ya Sokabet kuwawezesha washiriki wenye umri wa kuanzia miaka 18 kubet, pia inayo nafasi ya kukuza michezo kwa kuwekeza katika taasisi mbalimbali mfano kwa kuanzia imeanza na soka.
  Washambuliaji wapya ya Maji Maji, Danny Mrwanda (kulia) na Jerry Tegete (kushoto) kwenye wakiwa na jezi za Sokabet

  “Kama ambavyo Serikali ya Tanzania imekuwa ikisisitiza kuhusu kutoa ajira na kulipa kodi, kupitia Sokabet washindi watakaonufaika na mamilioni ya shilingi watapata nafasi ya kupewa elimu jinsi ya kutumia fedha hizo kujiajiri na kuendeleza miradi yao iliyopo au ambayo itaanzishwa kutokana na fedha watakazopata huku kila fedha za ushindi zikilipiwa kodi kwa mujibu wa sheria za nchi,”amesema Ruhinda. 
  Amesema ndani ya Sokabet kuna michezo mingi ya kubashiri ikiwemo Mpira wa Miguu wa Kimarekani, Baseball, Kikapu, Kriketi, Gofu, Mpira wa mikono, Mpira wa Magongo kwenye Mabarafu, Nbio za Gari, Raga, Tenisi, Mpira wa Wavu na Ndondi.
  Sokabet imezinduliwa rasmi leo kwenye hoteli ya Courtyard sambamba na kutaja udhamini wao kwa Maji Maji na washiriki wake wanatakiwa kubashiri matokeo kupitia tovuti yao ya www.sokabet.co.tz ili kuvuna fedha nyingi hadi shilingi milioni 100 kwa kubet kwa shilingi 1,000 tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAJI MAJI WAPATA UDHAMINI MILIONI 150 KWA MWAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top