• HABARI MPYA

  Sunday, September 17, 2017

  AZAM FC YAANZISHA TUZO ZA WACHEZAJI WAKE BORA WA MWEZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC, imeanzisha tuzo za Wachezaji Bora wa Mwezi na hatimaye Wachezaji Bora wa Msimu.
  Taarifa ya Azam FC leo imesema kwamba klabu inawapa fursa mashabiki wa timu hiyo ya kuwatunuku wachezaji wao wapendwa kila mwezi wakati wa mechi za mashindano.
  "Tuzo hizo ni maalumu kabisa inayodhaminiwa na Benki ya NMB ambao ni wadhamini wetu wakuu, inayokwenda kwa jina la ‘NMB Player of the Month’, ambayo itatolewa kila mwezi kwa mchezaji bora aliyefanya vizuri kwa mwezi husika,".
  Winga Mghana wa Azam FC, Enock Atta Agyei akimiliki mpira mbele ya beki wa Simba, Erasto Nyoni Jumamosi ya wiki iliyopita timu hizo zikitoka sare ya 0-0 

  Kwa kuanza rasmi mchakato, wakati Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiwa imeanza rasmi Agosti 26 kwa Azam FC kuichapa Ndanda bao 1-0, mashabiki wamepewa fursa ya kumchagua mchezaji bora wa mwezi huo uliopita.
  Tuzo hiyo ya kwanza itatolewa wiki ijayo Septemba 23 mwaka huu, kabla ya kuanza mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Lipuli utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuanzia saa 1.00 usiku.
  Aidha, ujio wa tuzo hizo haujawaacha mbali timu ya vijana ya Azam FC (Azam FC U-20), kwani nao watatunukiwa kila mwezi kama ilivyo kwa timu kubwa.
  Tuzo za Azam B zinadhaminiwa na wadhamini wetu wengine maji safi ya Uhai Drinking Water yanayokata kiu yako na kuondoa uchovu kutoka Bakhresa Food Products, tuzo hiyo itaitwa ‘Uhai Player of the Month.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAANZISHA TUZO ZA WACHEZAJI WAKE BORA WA MWEZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top