• HABARI MPYA

    Monday, March 14, 2016

    TENGA AUKWAA URAIS WA HESHIMA TFF

    Na Somoe Ng’itu, TANGA
    ALIYEKUWA Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, ameteuliwa kuwa Rais wa heshima wa shirikisho hilo na wajumbe wa mkutano mkuu waliokutana jana jijini hapa. 
    Jamal Malinzi, Rais wa TFF, aliwasilisha jina la Tenga katika mkutano huo ili wajumbe kulipigia kura na kutokana na mchango wa kiongozi huyo alipitishwa bila kupingwa. Malinzi alisema kwamba kamati ya utendaji ilifikia uamuzi wa kuliwasilisha jina la Tenga kutokana na kuheshimu na kuthamini mchango wake katika soka tangu alipokuwa mchezaji na kiongozi kwenye ngazi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. 
    Marais; Leodegar Tenga (kushoto) akiwa na Jamal Malinzi (kulia)

    Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo, alitoa sifa za Tenga na kueleza kwamba ameiwakilisha vyema bendera ya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kiwango cha kimataifa. 
    Kasongo alisema mbali na kuiongoza Taifa Stars katika fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1980 huko Lagos, Nigeria, Tenga akiwa Rais wa TFF aliweka misingi mizuri ya utawala bora. Rais huyo wa heshima aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania, BMT, Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Tanzania (CECAFA) na sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF(. Tenga pia aliwahi kuzichezea Yanga na Pan African zote za Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TENGA AUKWAA URAIS WA HESHIMA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top