• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 30, 2016

  UJERUMANI YAIFUMUA ITALIA 4-1, UFARANSA YAIPIGA 4-2 URUSI

  Mario Gotze wa Ujerumani akipambana katikati ya Matteo Darmian (kushoto) na Alessandro Florenzi kulia) wa Italia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa usiku huu Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich. Ujerumani imeshinda 4-1, huo ukiwa ushindi wake wa kwanza dhidi ya Itali baada ya miaka 20, mara ya mwisho waliifunga Azzuri 2-0 Juni mwaka 1995. Mabao ya Ujerumani usiku huu yamefungwa na Toni Kroos, Mario-Gotze, Jonas Hector na Mesut Ozil, wakati la Italia limefungwa na Stephan El Shaarawy PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  Kiungo wa Leicester City, N'Golo Kante akifumua shuti kuifungia Ufaransa bao la kwanza dakika ya nane katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Urusi usiku huu Uwanja wa Stade de France katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa akisherehekea kutimiza miaka ya 25 ya kuzaliwa. Mabao mengine ya Ufaransa yamefungwa na Andre-Pierre Gignac, Dimitri Payet na Kingsley Coman, wakati ya Urusi yamefungwa na Alexander Kokorin na Yuri Zhirkov PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UJERUMANI YAIFUMUA ITALIA 4-1, UFARANSA YAIPIGA 4-2 URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top