• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 29, 2016

  ZIMBABWE YAIFUMUA 4-0 SWAZILAND KUFUZU AFCON

  TIMU ya taifa ya Zimbabwe imepata ushindi mwingine mnono katika mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika Kundi L baada ya kuilaza Swaziland mabao 4-0 Jumatatu Uwanja wa Taifa mjini Harare.
  Mabao ya Zim yamefungwa na Knowledge Musona kwa penalti dakika ya 53, Costa Nhamoinesu anayechezea Sparta Prague ya Jamhuri ya Czech dakika ya 59, Evans Rusike na Khama Billiat wanaocheza Afrika Kusini.
  Zimbabwe sasa inafikisha ponti nane, Swaziland inabaki na pointi tano na Malawi na Guinea kila moja ina pointi mnili.
  Jamhuri ya Afrika ya Kati imepanda kileleni mwa Kundi B baada ya kuifunga Madagascar mabao 2-1 mjini Bangui.

  Nyota wa Malagasy, Faneva Ima Randriatsima anayecheza Daraja la Pili UIfaransa ndiye aliyeifungia timu yake Uwanja wa Barthelemy Boganda, wakati mabao ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yamefungwa na Salif Keita na Moussa Limane.
  Jamhuri ya Afrika ya Kati sasa inafikisha pointi saba baaada ya ushindi huo, ikiwa mbele ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi sita, Angola nne na Madagascar mbili.
  Mali imeiondoa Benin kileleni mwa Kundi C baada ya bao pekee la Mustapha Yatabare dakika za lala salama kuwapa ushindi wa 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea Uwanja wa Nuevo Estadio de Malabo.
  Wakati Mali inafikisha pointi 10 na Benin nane, Equatorial Guinea inabaki na pointi moja na kupoteza matumaini ya kufuzu.
  Mabao matatu ya Mohamed Zubya yameisaidia Libya kuilaza Sao Tome e Principe 4-0 katika mchezo wa Kundi F uliochezwa Cairo kwa sababu ya Libya wamefungiwa kucheza nyumbani.
  Morocco inayofundishwa na Herve Renard inaongoza kundi hilo kwa pointi zake tisa, huu Cape Verde ikifuatia kwa pointi zake sitana Libya naSao Tome kila moja ina pointi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZIMBABWE YAIFUMUA 4-0 SWAZILAND KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top