• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 25, 2016

  MASHABIKI WAIPOKEA KWA 'VISINGELI' STARS

  Mashabiki wa kikundi cha kuisapoti Taifa Stars wakicheza kwa usiku wa manane jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam wakati wa kuipokea timu yao ya taifa ikirejea kutoka Chad ambako Jumatano iliwafunga wenyeji 1-0 katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017
  Mashabiki walicheza ngoma zao kwa furaha kupongeza wachezaji na timu
  Wake kwa waume walijitokeza Uwanja wa Ndege usiku wa jana kuipokea Taifa Stars kwa furaha
  Katikati ni mwigizaji nyota, Dk Cheni akiwa na mmoja wa viongozi wa kikundi cha kuisapoti Taifa Stars, Papa Ziota (kushoto)
  Hadi ma- ustadh walikuwepo jana Uwanja wa ndege kuipokea Taifa Stars ya Tanzania
  Akina mama hawa waliwaacha waume zao vitandani kwa ajili ya Taifa Stars
  Vijana nao hawakuwa nyuma katika mapokezi hayo, waliacha starehe zote za kipindi hiki cha kuelekea Pasaka

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHABIKI WAIPOKEA KWA 'VISINGELI' STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top