• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 28, 2016

  BLACKWELL 'ANAPUMULIA MASHINE' BAADA YA KIPIGO CHA EUBANK

  BONDIA mkongwe Chris Eubank alitaka sana kuokoa maisha ya bonduia chipukizi, Nick Blackwell juzi Uwanja wa Wembley, lakini refa alikaidi.
  Mbabe huyo wa zamani alimuambia refa kusimamisha pambano wakati mwanawe, Chris Eubank anamuadhibu vibaya mpinzani wake, Blackwell ambaye sasa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi tangu baada ya pambano.
  Nick Blackwell, mwenye umri wa miaka 25 ambaye damu ilivujia kwenye ubongo baada ya kipigo hicho, alikimbizwa hospitali baada ya kutolewa ulingoni kwa machela Uwanja wa Wembley na tangu juzi yuko chini ya uanfalizi maalum.
  Eubank Sr aliyekuwa pembezoni mwa ulingo kama kocha wa mwanawe Jumamosi, angeweza kuokoa maisha ya Blackwell baada ya kumuambia mwanawe ampige mwilini mpinzani wake badala ya usoni alipoumia vibaya katika raundi mbili za mwisho.
  Pia alipanda ulingoni kumfuata refa Victor Loughlin kumuambia avunje pambano.


  Nick Blackwell, (kulia) akiwa amechafuka damu usoni kwa kipigo cha Chris Eubank Jr PICHA ZAIDI GONGA HAPA

   

  Hatimaye pambano hilo lilisimamishwa raundi ya tisa baada ya daktari wa pembeni ya ulingo kumshauri refa kwamba jicho la kushoto la bingwa mtetezi, Blackwell lilikuwa halioni tena na Eubank Jr, mwenye umri wa miaka 26 akabeba taji la uzito wa Middle Uingereza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BLACKWELL 'ANAPUMULIA MASHINE' BAADA YA KIPIGO CHA EUBANK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top