• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 28, 2016

  JUMA ABDUL: MECHI ZA AL AHLY PATACHIMBIKA DAR MPAKA CAIRO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI hodari wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amesema kwamba mechi za hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly ya Misri zitakuwa ‘za kufa mtu’.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE katika mahojiano maalum jana Dar es Salaam,  Juma Abdul amesema kwamba Yanga ya sasa ni bora zaidi tofauti ya miaka miwili iliyopita. 
  “Tunakwenda kukutana na timu ambayo ni kubwa, inafahamika, sisi kama Yanga tu mwaka juzi tumecheza nayo ikatutoa kwa taabu kwa penalti baada ya kila timu kushinda 1-0 nyumbani kwake,” amesema. 
  Juma Abdul (kushoto) amesema mechi na Al Ahly zitakuwa za kufa mtu Dar na Cairo

  “Miaka miwili baadaye tunakutana nayo tena, wazi itakuwa mechi ya ushindani sana.
  Unaweza kuona Yanga vimeongezeka vitu kutoka Yanga ile iliyocheza na Al Ahly mara ya mwisho, hatujui na upande wao, ila nadhani sasa ndiyo tutawatazama ili kuwajua wakoje,”ameongeza. 
  Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Al Ahly Aprili 9 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya kurudiana Aprili 19 mjini Cairo.
  (Usikose makala maalum ya mahojiano na Juma Abdul kesho)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JUMA ABDUL: MECHI ZA AL AHLY PATACHIMBIKA DAR MPAKA CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top