• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 29, 2016

  YANGA KAMBINI LEO KUJIANDAA NA WIKI NGUMU HAIJAWAHI KUWATOKEA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC wanaingia kambini leo katika hoteli moja ya kifahari mjini Dar es Salaam kujiandaa na wiki ngumu zaidi ambayo hawajawahi kukutana nayo daima.
  Yanga watacheza mechi nne za mashindano matatu ndani ya siku 10, moja ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation, mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Yanga wataanza kumenyana na Ndanda FC ya Mtwara Alhamisi ya Machi 31 katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la TFF, kabla ya kucheza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar Aprili 3 na dhidi ya Mtibwa Sugar Apeili 6, kabla ya kumenyana na Al Ahly ya Misri Aprili 9 katika 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa.
  Yanga watacheza mechi nne za mashindano ndani ya siku 10

  Mechi zote ni muhimu kwa Yanga kushinda, na kutokana na Bodi ya Ligi ya TFF kuwakomalia wacheze viporo vyao vya Ligi Kuu wanajikuta katika wiki ngumu, ambayo hadi kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm ameilalamikia.
  Pamoja na kwamba mechi zote ni muhimu, lakini Yanga wanaipa uzito zaidi mechi dhidi ya Al Ahly, ambayo itachezeshwa na Denis Dembele atakayesaidiwa na Marius Donatien Tan na Moussa Bayere, wote wa Ivory Coast.
  Timu hizo zitarudiana Apirli 19 mjini Cairo, Misri na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, wakati atakayefungwa ataangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
  Mechi ya Cairo itachezeshwa na Mahamadou Keita atakayesaidiwa na Balla Diarra na Drissa Kamory Niare watakaoshika vibendera pembezoni mwa Uwanja, wote kutoka Mali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA KAMBINI LEO KUJIANDAA NA WIKI NGUMU HAIJAWAHI KUWATOKEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top