• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 25, 2016

  COMORO WASHINDA MECHI YA KWANZA TANGU WAANZE SOKA

  TIMU ya taifa ya Comoro imemaliza ukame wa siku 3084 za kusubiri ushindi kwenye mechi za kimataifa za mashindano, baada ya jana kuwafunga wageni Botswana 1-0 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika.
  Bao pekee la Ben Mohamed dakika ya 56 lkimemaliza wimbi la mechi 20 bila ushindiu kwa Comoro kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika tangu mwaka 2007, wakati walipofungwa 6-2 na Madagascar katika mchezo wao wa kwanza wa kimataifa.
  Comoro jana wameshinda mechi ya kwanza ya mashindano ya kimataifa

  Mara tu baada ya Comoro kupata bao hilo, mvua kubwa ikamwagika Uwanja wa Sheikh Said Mohamed wenye kuchukua mashabiki 5,000 katika mchezo huo wa Kundi D. Comoro sasa inashika nafasi ya pili pamoja na Burkina Faso na Botswana kwa kila timu kuwa na pointi tatu, nyuma ya vinara Uganda wenye pointi sita.
  Wakati huo huo, beki wa zamani wa Everton na Liverpool, Abel Xavier ameanza vibaya kazi baada ya Msumbiji kufungwa 3-1 ugenini na Ghana.
  Liberia imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya Djibouti na Madagascar imelazimishwa sare na Jamhuri ya Afrika ya Kati jana pia. Mabao ya Ghana yamefungwa na Abdul-Majeed Waris, John Boye na Jordan Ayew Uwanja wa Accra Sports.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: COMORO WASHINDA MECHI YA KWANZA TANGU WAANZE SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top