• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 30, 2016

  GARY NEVILLE ATUPIWA MABEGI YAKE VALENCIA

  KOCHA Gary Neville amefukuzwa Valencia ya Hipania wakati zikiwa zimebaki mechi nane msimu kumalizika. 
  Msaidizi wa zamani wa Rafa Benitez alipokuwa Liverpool, Pako Ayestaran, ambaye aliteuliwa kuwa kocha wa pili wa Neville Januari, ameteuliwa kuwa mrithi wake hadi mwishoni mwa msimu, wakati Phil Neville anatarajiwa kuendelea kubaki klabuni kama sehemu ya makocha wa timu ya Ayesteran.
  Neville alitarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu, lakini mmiliki wa Valencia, Peter Lim uvumilivu umemshinda kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya, hivyo amembwaga mapema.
  Kwa sasa Valencia ina pointi sita zaidi kutoka eneo la kushuka daraja na wasiwasi ni kwamba Gary Neville akibaki timu inaweza kuporomoka zaidi ndani ya mechi nane zilizobaki kuelekea mwishoni mwa msimu. 

  Beki wa zamani wa kulia wa Manchester United, Gary Neville amefukuzwa Valencia ya Hispania PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GARY NEVILLE ATUPIWA MABEGI YAKE VALENCIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top