• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 27, 2016

  RAGE 'ATUMBUA JIPU' SIMBA FUBA LA OKWI

  Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage (pichani kushoto) amesema anashukuru fedha za usajili wa mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Mganda Emmanuel Okwi zimewasili, hivyo waliosema amekula wamepata majibu ya maswali yao.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana mjini Dar es Salaam, Rage alisema kwamba anashukuru sana kusikia fedha hizo zimewasili wiki mbili zilizopita, hivyo kwa sasa hakuna mjadala wa suala hilo.
  Rage alisema tayari klabu ya Etoile du Sahil imeilipa Simba kiasi cha dola za Kimarekani 300,000 ambayo ni zaidi ya Sh. Milioni 600 kwa fedha ya Tanzania.
  Emmanuel Okwi (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe (kulia)

  Alisema licha ya fedha hizo kuingizwa, lakini Simba imepata dola 19,000 zaidi ambayo ni sawa na Sh.milioni 39, kama sehemu ya usumbufu kwa fedha hizo kucheleweshaa kulipwa.
  Alisema, kupitia fedha hizo ambazo wamepata klabu hiyo ina uwezo wa kujenga Uwanja wa kisasa na kupata Nyumba nzuri za kuishi wachezaji wao, kama sehemu ya kambi ya timu hiyo, wanapokuwa wanakabiliwa na mashindano mbalimbali.
  Rage alisema ni kitu kizuri kwake kupatikana kwa fedha hizo na kutasaidia yeye na uongozi wake uliopita wawe wameshinda sataka hilo ambalo limeenda kwa muda mrefu kutokana na wanachama kutokujua kama klabu imepata au la.
  Alipotafutwa Rais wa Simba, Evans Aveva kuzungumzia suala hilo, alisema yeye hajui kama fedha hizo zimewasili na hawezi kulizungumzia suala hilo kwa sasa, kwa sababu kwa sasa wanaangalia zaidi Ligi Kuu ili waweze kuchukua ubingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAGE 'ATUMBUA JIPU' SIMBA FUBA LA OKWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top