• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 27, 2016

  RWANDA NA UGANDA ZOTE ZAPIGWA MBIO ZA AFCON 2017

  Rwanda wamepoteza mechi ya ugenini kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon baada ya kufungwa 1-0 na Mauritius jana
  UGANDA na Rwanda zimepoteza mechi za ugenini kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika jana. Mauritius imeiiunga Rwanda 1-0 Uwanja wa Anjalay mjini Belle Vue, bao pekee la beki Francis Rasolofonirina dakika ya 59, wakati Uganda imefungwa 1-0 na Burkina Faso mjini Ouagadougou.
  Mechi nyingine za jana, Senegal imeifunga 2-0 Niger Uwanja wa Stade Leopold Sedar Senghor mjini Dakar, Morocco imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya Cape Verde mjini Praia, wakati Cameroon imelazimishwa sare ya 2-2 na Afrika Kusini, DRC imeifunga 2-1 Angola Uwanja wa Stade des Martyrs, Kinshasa, wakati Burundi imefungwa 3-1 nyumbani na Namibia Uwanja wa Prince Louis Rwagasore, Buumbura na Shelisheli imeifunga 2-0 Lesotho Uwanja wa Stade Linite.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RWANDA NA UGANDA ZOTE ZAPIGWA MBIO ZA AFCON 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top