• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 31, 2016

  KAPOMBE APIGA MBILI, AZAM YAING’OA PRISONSKOMBE LA TFF

  Na Mwandishi Weu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kuitandika mabao 3-1 Prisons ya Mbeya jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Azam FC walipata bao lao lao kwanza dakika ya tisa, mfungaji Shomary Kapombe aliyefumua shutibaada ya kazi nzuri ya mshambuliaji wa Burundi, Didier Kavumbagu.
  Mshambuliaji chipukizi, Jeremiah Juma akaisawazishia Prisons FC dakika ya 30 akitumia bahati mbaya ya beki wa Azam FC, Aggrey Morris kuteleza na kuanguka chini naye akawahi mpira na kumtungua kipa Aishi Manula.
  Kipindi cha pili, Kapombe tena aliifungia Azam FC bao la pili dakika ya 50 akimalizia pasi ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
  Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nahodha John Bocco, aliipatia Azam FC bao la tatu dakika ya 86.
  Azam FC sasa inaungana na Mwadui FC ya Shinyanga iliyoitoa Geita Gold na Yanga iliyoitoa Ndanda FC, wakati Robo Fainali ya mwisho itakuwa kati ya Simba na Coastal Union Aprili 11, Uwanja wa Taifa. 
  Kikosi cha Azam FC: Aishi Manula, Shomary Kapombe/Farid Mussa dk80, Waziri Salum/Frank Domayo dk46, Aggrey Morris, Serge Wawa, Erasto Nyoni, Kipre Balou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Ramadhani Singano ‘Messi’, John Bocco/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk60 na Didier Kavumbagu.
  Prisons: Beno Kakolanya, Salum Kimenya, Laulian Mpalile, James Mwosote, Lugano Mwangama,  Jumanne Elfadhil,  Lambarty Sabiyanka/Meshack Suleiman dk62, Freddy Chudu/Baraka Majogoo dk71, Mohamed Mkopi,  Jeremiah Juma/Frank William dk74 na Benjamin Asukile.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAPOMBE APIGA MBILI, AZAM YAING’OA PRISONSKOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top