• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 26, 2016

  SERGE WAWA MECHI 70 AZAM BAO MOJA TU!

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI raia wa Ivory Coast wa Azam FC, Serge Pascal Wawa (pichani kulia) jana amecheza mechi yake ya 70 tangu ajiunge na Azam FC, lakini amefunga bao moja tu.
  Wawa aliyejiunga na Azam FC mwaka juzi kutoka El Merreikh ya Sudan alicheza kwa dakika 45 jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers ya Daraja la kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Na alimpisha beki mzalendo Aggrey Morris kipindi cha pili wakati Azam FC inaongoza 3-0, mabao ya viungo Ramadhan Singano ‘Messi’, Kipre Balou Muivory Coast pia na mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbagu.
  Azam iliongeza mabao matatu kipindi cha pili yaliyofungwa na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, winga Khamis Mcha ‘Vialli’ na kinda Shaaban Idd, wakati Rangers ilipata bao lao la kufutia machozi dakika ya 73 kupitia kwa nyota wao Cosmas Lewis kwa mkwaju wa penalti baada ya Aggrey Morris kucheza rafu kwenye boksi.
  Serge Wawa analingana na beki wa Yanga Mtogo Vincent Bossou aliyefunga bao moja pia katika mechi 24 wakati beki mwingine wa kati wa kigeni, Mganda Juuko Murshid katika mechi 53 alizocheza Simba SC amefunga mabao mawili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERGE WAWA MECHI 70 AZAM BAO MOJA TU! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top