• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 31, 2016

  SUNDERLAND YAMFUKUZA EBOUE KWA UDHULIMISHI

  KLABU ya Sunderland imemfukuza beki Emmanuel Eboue baada ya siku 22 tangu imsajili kufuatia taarifa za kufungiwa kwake mwaka mmoja kwa kushindwa kumlipa wakala wake wa zamani.
  Mapema asubuhi ya leo, FIFA imesema leo nyota huyo wa zamani wa Arsenal mwenye umri wa miaka 32 hataruhisiwa kujishughulisha na soka hadi atakapomlipa Sebastien Boisseau, anayemdai kiasi cha Pauni Milioni 1.
  Sunderland imechukua hatua za haraka kwa kumvunjia Mkataba Eboue, licha ya kwamba alikuwa hajaripoti kuanza kazi kwenye klabu hiyo baada ya kujiunga nayo kama mchezaji huru Machi 9.
  Emmanuel Eboue amefungiwa mwaka mmoja na FIFA hadi hapo atakapomlipa wakala wake wa zamani PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Pamoja na hayo, Eboue anaweza kurejeshwa kikosini Sunderland iwapo atamalizana na wakala wake kwa kulipa deni hilo ndani ya wiki mbili zijazo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUNDERLAND YAMFUKUZA EBOUE KWA UDHULIMISHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top