• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 27, 2016

  TFF YASHITUKIA USHINDI WA 16-0 LIGI YA MKOA

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limekiagiza Chama cha Soka Katavi (KRFA) kufanya uchunguzi juu ya matokeo ya kumpata bingwa wa ligi ya mkoa huo iliyomalizika wikiendi hii kabla ya kutangaza Bingwa wa Mkoa wa Katavi.
  TFF imeagiza KRFA kuziagiza kamati zake kufanya uchunguzi juu ya matokeo ya mwisho baada ya Stand FC kuibuka na ushindi wa mabao 16-0 dhidi ya Kazima FC.
  Kabla ya mchezo huo wa mwisho, klabu ya Nyundo FC ilikua inangoza kwa kuwa na pointi 21 na magoli 24 ya kufunga, na klabu ya Stand FC ilihitajia ushindi wa mabao 13 ili kuweza kuwa bingwa wa mkoa wa Katavi, hali inayoleta hofu ya kuwepo upangwaji matokeo katika ushindi wa Stand FC wa mabao 16-0 dhidi ya Kazima FC.
  KRFA haitaruhusiwa kutangaza bingwa wa mkoa hadi uchunguzi ukamilke na TFF ijiridhishe na uchunguzi huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YASHITUKIA USHINDI WA 16-0 LIGI YA MKOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top