• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 22, 2016

  KAPOMBE: NITARUDI ULAYA, ILA SI KINYONGE

  Na Prince Akbar, ADDIS ABABA
  BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Shomary Salum Kapombe amesema kwamba atarudi Ulaya iwapo atapata ofa ya kuanzia timu ya Daraja la Kwanza, lakini si chini ya hapo.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE mjini Addis Ababa leo, Kapombe anayechezea Azam FC amesema kwamba kucheza Ulaya ni ndoto ya kila mchezaji wa Afrika.
  “Watu walinilaumu sana mwaka juzi nilipoondoka AS Cannes (ya Ufaransa) kuja Azam, lakini hawakujua tu. Ni mambo mengi ambayo siwezi kusema,”amesema Kapombe.
  Hata hivyo, beki huyo wa zamani wa Simba amesema alichojifunza ni kwamba hatakubali ofa yoyote ya kwenda Ulaya kujiunga na timu ya chini ya Daraja la Kwanza.
  Shomary Kapombe amesema atarudi Ulaya lakini kwa timu ya chini ya Daraja la Kwanza
  “Mimi ni mchezaji wa kimataifa, nina nafasi timu yangu ya taifa na klabu yangu inacheza mashindano makubwa, nina uzoefu wa kutosha kucheza popote,”amesema na kuongeza; “Wakala anayetaka kunipa dili la Ulaya, basi liwe la klabu ya Daraja la kwanza, au Ligi Kuu,”amesema.Pamoja na hayo, Kapombe amesema hawezi kuondoka Azam FC kujiunga na klabu nyingine yoyote Tanzania.
  “Ninafurahia maisha Azam FC, upendo na maslahi bora, ninataka nini zaidi, nikiondoka hapa nimepata timu nayoitaka Ulaya,”amesema kapombw aliyewahi kuchezea AS Cannes ya Daraja la Nne Ufaransa kwa miezi kadhaa mwaka 2013.

  Kapombe kulia akiwa na mchezaji mwenzake wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu leo mjini Addis Ababa

  Kapombe amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu, kuanzia katika klabu yake, Azam FC hadi timu ya taifa.

  Kwa sasa ndiye beki aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi Kuu kuliko, akiwa ametikisa nyavu mara saba, kiasi cha kuwazidi baadhi ya washambuliaji wa klabu yake. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAPOMBE: NITARUDI ULAYA, ILA SI KINYONGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top