• HABARI MPYA

    Thursday, March 31, 2016

    MALINZI AHOFIA KARUME KUPIGWA MNADA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (pichani kushoto) amesema kwamba ana wasiwasi Uwanja wa Karume, unaweza kupigwa mnada na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
    Hiyo inafuatia TRA kukamata magari matano ya TFF kutokana na deni la kodi Sh. Bilioni 1 Milioni 118 ambazo ni malimbikizo tangu mwaka 2010, wakati TFF ikiwa chini ya Rais Leodegar Tenga.
    “Kwa kweli hali mbaya, na sitashangaa hata kesho Uwanja wa Karume nao ukipigwa mnada, kwa sababu magari waliyokamata thamani yake haifiki deni wanalodai,”amesema Malinzi leo Dar es Salaam. 
    Ofisa wa TRA, Richard Kayombo amesema wamekamata magari hayo ili kuwapa shinikizo TFF waweze kulipa madeni hayo.
    Amesema deni hilo la Sh. Bilioni 1 na Milioni 118 ni malimbikizo ya kodi mbalimbali kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, zikiwemo za VAT na mishahara ya wafanyakazi wake.
    “Ikumbukwe awali tulikamata akaunti zao kwa sababu deni lilifikia Bilioni 1. 6 na baada ya kupunguza deni tukawaachia akaunti zao, lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano,”amesema Kayombo.
    Ofisa huyo wa TRA amesema magari yote yaliyokamatwa, likiwemo basi la wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars yapo kwenye kampuni minada ya Yono.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AHOFIA KARUME KUPIGWA MNADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top