• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 22, 2016

  MALAWI YATAJA KIKOSI CHA KUIVAA GUINEA

  KOCHA wa Malawi, Ernest Mtawali ametaja wachezaji 20 kwa ajili ya michezo miwili ya nyumbani na ugenini Kundi L kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Guinea.
  Mtawali ameita wachezaji 13 wanaocheza nje hususan kutoka klabu za Msumbiji na Afrika Kusini na The Flames itasafiri kwenda Conakry kumenyana na Guinea Ijumaa ya Machi 25 kabla ya kurudi kuwapokea wapinzani wao hao mjini Blantyre siku nne baadaye.
  Kikosi kamili cha Malawi ni makipa; Brighton Munthali (Silver Strikers), John Soko (Blue Eagles)
  Mabeki; Limbikani Mzava (Mpumalanga Black Aces, Afrika Kusini), Stanley Sanudi (Be Forward Wanderers), Francis Mlimbika (Be Forward Wanderers), Miracle Gabeya (Nyasa Big Bullets), Wonderful Jeremani (Silver Strikers), Yamikani Fodya (Nyasa Big Bullets), John Lanjesi (Nyasa Big Bullets), Harry Nyirenda (Black Leopards).
  Viungo; Chimango Kayira (Costa de Sol, Msumbiji), Robert Ng'ambi (Platinum Stars, Afrika Kusini), Joseph Kamwendo (Liga Desportivo de Maputo, Msumbiji),Micium Mhone (Jomo Cosmos, Afrika Kusini), John Banda (Ferroviaro de Nampula, Msumbiji), Isaac Kaliati (Be Forward Wanderers)
  Washambuliaji; Chiukepo Msowoya (Nyasa Big Bullets), Gabadinho Mhango (Golden Arrows, Afrika Kusini), Zicco Mkandawire (Liga Desportivo de Maputo, Msumbiji), Schumacher Kuwali (Ferroviaro de Nampula, Msumbiji).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALAWI YATAJA KIKOSI CHA KUIVAA GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top