• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 24, 2016

  STARS NA CHAD KATIKA PICHA JANA

  Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta (kulia) akipambana na beki wa Chad katika mchezo wa Kundi G, kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 jana Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini D'jamena. Taifa Stars ilishinda 1-0

  Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akimvisha kanzu ya kisigino watoto wa bongo wanasema 'kizungu' beki wa Chad jana

  Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akigombea mpira na beki wa Chad jana

  Winga wa Taifa Stars, Farid Mussa akimtoka beki wa Chad jana

  Kiungo wa Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto akitafuta maarifa ya kuwapita wachezaji wa Chad jana

  Beki wa kulia wa Taifa Stars, Shomary Kapombe (kushoto) akitafuta maarifa ya kumpira beki wa Chad jana

  Mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu akimruka kipa wa Chad baada ya kudaka mpira

  Kiungo wa Taifa Stars, Jonas Mkude akimtoka mchezaji wa Chad huku akifikiria pia namna ya kumpita mchezaji mwingine wa timu hiyo jana

  Kiungo wa Taifa Stars, Himid Mao (kulia) akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa Chad jana 

  Kikosi cha Taifa Stars kilichlifunga 1-0 Chad jana mjini D'jamena

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS NA CHAD KATIKA PICHA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top