• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 20, 2016

  THOMAS ULIMWENGU 'AMLIZA' NOOIJ LUBUMBASHI

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu (pichani kushoto) leo amemtia simanzi kocha wake wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij.
  Hiyo ni baada ya Ulimwengu leo kuiongoza klabu yake, TP Mazembe kuitoa St George ya Ethiopia inayofundishwa na Nooij katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Ulimwengu aliyeingia dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Rogger Assale ameisaidia timu yake kushinda 1-0 dhidi ya St George Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, DRC bao pekee la Jonathan Bollingi kwa penalti.
  Na kwa matokeo hayo, Mazembe inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kutoa sare ya 2-2 Ethiopia wiki iliyopita.
  Mart Nooij alikuwa kocha wa Taifa Stars kabla ya kurejea St George ya Ethiopia iliyotolewa na Mazembe Ligi ya Mabingwa leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: THOMAS ULIMWENGU 'AMLIZA' NOOIJ LUBUMBASHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top