• HABARI MPYA

    Tuesday, March 29, 2016

    CAF YAMTUPA NIYONZIMA JUKWAANI YANGA NA AL AHLY, TAMBWE, KAMUSOKO, NGOMA NAO!

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Haruna Niyonzima hatacheza mchezo wa kwanza wa 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri Aprili 9, kutokana na kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kumbana.
    Niyonzima alipewa kadi za njano katika mbili mfululizo za Raundi ya Kwanza dhidi ya APR ya kwao, Rwanda mjini Kigali Yanga ikishinda 2-1 na Dar es Salaam timu hizo zikitoka 1-1.
    Kwa maana hiyo, Haruna atakuwa jukwaani kabisa siku hiyo Yanga ikipigania ushindi mzuri wa nyumbani, kabla ya kurejea kwa ajili ya mchezo wa marudiano Aprili 19 mjini Cairo.
    Haruna Niyonzima hatacheza dhidi ya Al Ahly Aprili 9 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Aidha, washambuliaji tegemeo wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma wote wapo hatarini kuukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Ahly mjini Cairo.
    Nyota hao pamoja na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamuko walionyeshwa kadi za njano katika mechi dhidi ya APR mjini Dar es Salaam, maana yake ikitokea bahati mbaya ya kuonyeshwa pia kadi na Aprili 9 Uwanja wa Taifa, hawatasafiri kwenda Misri.
    Yanga imeingia kambini jana katika hoteli moja ya kifahari mjini Dar es Salaam kujiandaa na wiki ngumu ya kucheza mechi nne za mashindano matatu, moja ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation, mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Yanga wataanza kumenyana na Ndanda FC ya Mtwara Alhamisi ya Machi 31 katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la TFF, kabla ya kucheza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar Aprili 3 na dhidi ya Mtibwa Sugar Apeili 6, kabla ya kumenyana na Al Ahly ya Misri Aprili 9.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAMTUPA NIYONZIMA JUKWAANI YANGA NA AL AHLY, TAMBWE, KAMUSOKO, NGOMA NAO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top