• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 26, 2016

  YONDAN, KAZIMOTO WAJIFUA NA STARS LEO

  Na Prince Akbar, ADDIS ABABA
  WACHEZAJI wawili tegemeo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, beki Kevin Yondan na kiungo Mwinyi Kazimoto wote wamefanya mazoezi leo baada ya kupata nafuu ya maumivu yao.
  Yondan wa Yanga na Mwinyi wa Simba zote za Tanzania, wote hawakufanya mazoezi jana baada ya kuwasili Dar es Salaam Alfajiri ya Ijumaa wakiwa wagonjwa kufuatia kuumia mjini Djamena Jumatano katika mchezo dhidi ya wenyeji, Chad.
  Taifa Stars ilishinda 1-0 dhidi ya Chad Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini D’jamena katika mchezo huo wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika, bao pekee la Nahodha, Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji dakika ya 30 akimalizia krosi ya Farid Mussa wa Azam FC.
  Kutoka kulia ni Mwinyi Kazimoto na Kevin Yondan mazoezini Uwanja wa Taifa leo 

  Kazimoto alishindwa kuendelea na mchezo baada ya dakika 45 tu, wakati Yondan pamoja na kumaliza dakika 90, lakini alipofika hotelini hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali usiku ambako alitibiwa na kurejea hoteli ya kifahari zaidi mjini D’jamena, Ledger Plazza ambako Taifa Stars walifikia.
  Sasa wana Mwanza hao, Yondan na Kazimoto wanaweza kuanza katika mchezo wa marudiano na Chad keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Taifa Stars imeendelea na mazoezi yake jioni ya leo chini ya makocha wake, Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kujiandaa na mechi dhidi ya Chad Jumatatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YONDAN, KAZIMOTO WAJIFUA NA STARS LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top