• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 27, 2016

  EUBANK AMPIGA MTU WEMBLEY HADI AKIMBIZWA HOSPITALI

  Nick Blackwell (kushoto) akiadhibiwa na Chris Eubank (kulia) katika pambano la la jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  BONDIA Chris Eubank Jnr ndiye bingwa mpya wa uzito wa Middle nchini Uingereza, baada ya kumshinda kwa Knockout (KO) raundi ya 10 mpinzani wake, Nick Blackwell Uwanja wa Wembley.
  Eubank Jnr alitawala pambano hilo hakupata mkisukosuko hata kidogo kutoka kwa mpinzani wake, na Daktari akasema Blackwell hawezi kuona tena baada ya kuchakazwa na makonde usoni.
  Bondia huyo wa Wiltshire ilibidi akimbizwe hospitali baada ya kuondolewa ulingoni kwa machela.  
  Bingwa wa dunia wa uzito wa juu, Tyson Fury ametweet; "Tumuombee dua Nick Blackwell tafadhali, amepelekwa hospitali, Mungu awe naye,". 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EUBANK AMPIGA MTU WEMBLEY HADI AKIMBIZWA HOSPITALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top