• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 26, 2016

  YANGA NA AL AHLY MAREFA WOTE WA MAGHARIBI DAR ES SALAAM NA CAIRO

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji Yanga SC na Al Ahly ya Misri Aprili 9, mwaka huu utachezeshwa na marefa kutoka Magharibi mwa Afrika.
  Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na waamuzi watakuwa Denis Dembele atakayepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera, Marius Donatien Tan na Moussa Bayere, wote wa Ivory Coast.
  Aidha, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewapanga pia waamuzi kutoka Magharibi mwa Afrika katika mchezo wa marudiano, Apirli 19 mjini Cairo, Misri.
  Al Ahly iliitoa Yanga mwaka juzi katika Ligi ya Mabingwa Afrika 

  Hao ni Mahamadou Keita atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Balla Diarra na Drissa Kamory Niare watakaoshika vibendera pembezoni mwa uwanja, wote kutoka Mali.
  Aidha, wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Afrika, Azam FC watamenyana na Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho wiki ya kwanza ya Aprili.
  Mchezo wa kwanza unatarajiwa kufanyika Aprili 10 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na utachezeshwa na marefa wa Afrika Kusini.
  Hao ni Daniel Frazer Bennett atakayepuliza filimbi na washika vibendera Zakhele Thusi Siwela na Thembisile Theophilus Windvoel.
  Mchezo wa marudiano Aprili 19 utachezeshwa na marefa wa Morocco, ambao ni Redouane Jiyed katikati, Mouhib Abdallah Filali na Essam Benbara pembeni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA NA AL AHLY MAREFA WOTE WA MAGHARIBI DAR ES SALAAM NA CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top