• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 31, 2016

  AZAM NA PRISONS CHAMAZI, YANGA NA NDANDA TAIFA

  ROBO Fainali ya michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye viwanja tofauti mjini Dar es Salaam.
  Azam FC watakuwa kwenye Uwanja wao wa Azam Complex, Chamazi, kuwakaribisha Prisons ya Mbeya, wakati Yanga SC nao watakua wenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mechi zote zikianza Saa 10:00 jioni.
  Robo Fainali ya mwisho itachezwa Aprili 11, Simba SC wakimenyana na Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Mwadui FC ndio timu pekee mpaka sasa ambayo imeshafuzu kwa hatua ya nusu fainali, baada ya kuwachapa Geita Gold kwa mabao 3 -0.
  Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) atawakilisha Tanzania mwakani kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM NA PRISONS CHAMAZI, YANGA NA NDANDA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top