• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 24, 2016

  HIZI SASA FUJO, PSG WAMTAKA STURRIDGE

  MATAJIRI wa Ufaransa, Paris Saint-Germain wanaitaka huduma ya mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 45, mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge.
  Msafara kutoka klabu hiyo ya Paris unatarajiwa kuwasili London kuhudhuria mechi kati ya England na Uholanzi Uwanja wa Wembley leo.
  Sturridge anatarajiwa kucheza sehemu ya mchezo huo baada ya kurejeshwa kikosini. Kocha wa PSG, Laurent Blanc atakuwa sokoni kusaka mshambuliaji mpya kutokana na Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani kuhofiwa kuwa mbioni kuondoka.
  Na Sturridge jina lake limo katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa PSG, ingawa amebakiza miaka mitatu katika Mkataba wake Merseyside. 

  Sturridge amekuwa katika kiwango kizuri Liverpool msimu huu tangu arejee uwanjani kufuatia kupona maumivu yake ya muda mrefu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HIZI SASA FUJO, PSG WAMTAKA STURRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top