• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 28, 2016

  IBRAHIMOVIC ATHIBITISHA SAFARI YA ENGLAND, ARSENAL WAMO

  MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic amethibitisha kupokea ofa za timu za Ligi Kuu ya England.
  Ibrahimovic anatarajiwa kuondoka Ufaransa mwishoni mwa msimu baada ya mkataba wake wa sasa na mabingwa wa nchi hiyo utakapomalizika na mbio za kuwania saini yake zimeanza.
  Arsenal na Chelsea, pamoja na West Ham, zote zinamtaka mchezaji huyo ahamie London, lakini Msweden huyo amethibitisha atatulia kutafakari ili kuchukua uamuzi sahihi.
  Akizungumza kuelekea mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Sweden na Jamhuri ya Czech, Ibrahimovic amesema: "Ndiyo, kuna timu zinanitaka Ligi Kuu ya England, naweza kuthibitisha hilo.
  Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic amethibitisha kutakiwa Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  "Ligi Kuu ya England ni ambayo wote duniani na mashabiki wanaizungumzia. Mambo mengi inabidi uyafikirie vizuri wakati nitakapofanya maamuzi mwishoni mwa msimu,".
  "Wakati utakapofika, wakati kete zipo mezani, hapo ndipo nitakapoamua wapi pa kwenda kutokana na kipi ninachotaka ndipo tutaona zaidi,".
  "Ni kama ndoa. Pande mbili zinatakiwa kuihitaji, siyo tu mmoja au mwingine. Kila upande unatakiwa kuitaka kama upande mwingine," amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: IBRAHIMOVIC ATHIBITISHA SAFARI YA ENGLAND, ARSENAL WAMO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top