• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 28, 2016

  SIMBA, TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA DHAIRA

  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uganda (FUFA) kaufuatia kifo cha mlinda mlango Abel Dhaira kilichotokea jana jijini Kampla.
  Katika salamu hizo za rambirambi, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki, FUFA kufuatia msiba Dhaira, na kusema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hiki cha maombelezo.
  Dhaira alifariki jana Jumapili kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa Kansa
  Wakati wa uhai wake Dhaira aliwahi kuidakia timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ na kuvichezea vilabu vya Express FC, URA (Uganda), AS Vita (Congo DR), Simba SC (Tanzania) na klabu ya BV Vestmannaeyjar ya Iceland.
  Abbel Dhaira (kushoto) siku za mwisho za uhai wake nchini Iceland

  Wakati huo huo: Klabu ya Simba nayo imesema imepokea kwa mshtuko taarifa ya msiba wa mchezaji wake wa zamani mganda Abel Dhaira.
  "Kwetu sisi ni pigo kubwa sana, ni msiba mzito sana, umetufanya tupate fadhaa kubwa, lakini hatuna la kufanya zaidi ya kumtakia mapumziko mema ya milele,".
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara amesema watamkumbuka sana Dhaira kwa uwezo wake wa kudaka krosi na nidhamu yake iliyokuwa mfano kwa wachezaji wote waliokuwepo kipindi kile.

  "Tunawaomba familia ya marehemu iwe na subira kwenye kipindi hiki kigumu sana kwao,"amesema Manara. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA, TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA DHAIRA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top