• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 23, 2016

  RAIS FIFA AISHUHUDIA SUDAN KUSINI IKIFA 2-1 NYUMBANI

  MABAO mawili ya dakika za lala salama yameipa ushindi wa 2-1 Sao Tome dhidi ya Libya wakati Guinea-Bissau imeibwaga Kenya ya kocha mpya, Samuel Okumbi 1-0 katika mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 leo.
  Rais mpya wa FIFA, Gianni Infantino ameishuhudia Sudan Kusini ikifungwa 2-1 nyumbani na Benin wakati Zambia imelazimishwa sare ya 1-1 Kongo Brazzaville.
  Faisal Al Badry aliifungia Libya bao la kuongoza katikati ya kipindi cha kwanza Uwanja wa 12 de Julho mjini Sao Tome, kabla ya wenyeji wakapata mabao mawili ndani ya dakika tano na kushinda dakika za mwishoni kupitia kwa Ahmed Al Terbi dakika ya 82 na Luis Leal dakika za majeruhi.

  Rais mpya wa FIFA, Gianni Infantino ameishuhudia Sudan Kusini ikifungwa 2-1 nyumbani na Benin 

  Bao pekee la Idrissa Camara dakika ya 19 limeipa ushindi wa 1-0 Guinea-Bissau dhidi ya Kenya, Zambia imetoa sare ya nyumbani Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola na Kongo, Winston Kalengo akianza kuwafungia wenyeji dakika ya 60, kabla ya Jordan Massengo kuwasawazishia wageni dakika ya 75.
  Infantino, aliyerithi nafasi ya Sepp Blatter FIFA alikuwepo Uwanja wa Juba wenyeji Sudan Kusini wakifungwa 2-1 na Benin, kiungo wa West Bromwich Albion ya England, Stephane Sessegnon akifunga bao la kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAIS FIFA AISHUHUDIA SUDAN KUSINI IKIFA 2-1 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top