• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 28, 2016

  CAMP NOU SASA JOHAN CRUYFF ARENA

  Johan Cruyff akiiongoza Barca kuingia Uwanja wa Nou Camp Januari 8, mwaka 1977 kumenyana na Rayo Vallecano katika mchezo wa La Liga PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  UHOLANZI NAO WAAMUA

  Chama cha Soka Uholanzi (KNVB) kimetangaza kwamba wataubadilisha jina Uwanja wa Amsterdam Arena na kuuita Johan Cruyff ili kumpa heshima yake mshindi huyo wa tuzo tatu za Ballon d'Or aliyefariki kwa ugonjwa wa saratani.
  Rais wa KNVB, Michael van Praag, amesema: "Siwezi kuchelewa kuubadilisha jina Uwanja wetu na kuwa Johan Cruyff Arena. Ni heshima kubwa tunaweza kumpa yeye,".
  BODI ya Wakurugenzi ya Barcelona itakutana Jumanne kujadili namna ya kumuenzi gwiji wake, Johan Cruyff, aliyefariki dunia wiki iliyopita.
  Kwa mujibu wa gazeti la michezo la kila siku Katalunya, Sport, ni kwamba dhamira ya Blaugrana ni kuubadili jina Uwanja wa Nou Camp na kuupa jina la gwiji huyo wa Uholanzi ambaye enzi za uhai wake alifanya kazi kama mchezaji na kocha.
  Cruyff aliyefariki dunia Alhamisi baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani akiwa na umri wa miaka 68, ameshinda mataji ya La Liga na Copa del Rey uwanjani hapo akiwa na Barca, kabla ya kutwaa mataji mengine kibao akiwa kocha likiwemo Kombe la Ulaya mwaka 1992.
  Barcelona inatafakari namna ya kumpa heshima ya kudumu Cruyff kutokana na mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo enzi za uhai wake.
  Mtoto wa kiume wa Cruyff, Jordi, ambaye kama baba yake amechezea Barca na Uholanzi, alikutana na Makamu wa Rais wa klabu, Jordi Cardoner kuanza kujadili mpangop huo Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAMP NOU SASA JOHAN CRUYFF ARENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top